Connect with us

Soka

Senzo C.E.O Yanga sc

Uongozi wa klabu ya Yanga sc umemtangaza Senzo Mazingiza kuwa mtendaji mkuu mpya wa klabu hiyo kwa kipindi chote cha mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo kutoka mfumo wa wanachama kwenda kwenye mfumo wa Hisa.

Senzo aliyekua mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc ambapo baadae alihamia Yanga sc ambapo alikua na mshauri mkuu wa mfumo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kukamilisha shughuli za kuhamisha mfumo kuwa wa kisasa ambapo kutakua na umiliki wa hisa.

Awali klabu ya Yanga sc iliendeshwa na Mwenyekiti Dk.Mshindo Msolla huku mtendaji mkuu akiwa na Kaimu Katibu mkuu Haji Mfikirwa  aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, atarudi kwenye nafasi yake ya Mkurugenzi wa Fedha na utawala wa Yanga SC

Katika mkutano na waandishi wa habari kumtambulisha Senzo katika nafasi hiyo,Uongozi wa Yanga sc Wamesisitiza kwasasa klabu hiyo inahitaji mtu aina ya Senzo ili kufika haraka katika mabadiliko yao.

Ikumbukwe kuwa Senzo Mazingiza ni mmoja kati ya watu wenye uzoefu katika utawala wa soka Afrika akiwa ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ngazi za juu za soka Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka