Wednesday, May 7, 2025
Home Makala Sakata Jipya Kocha Singida FG

Sakata Jipya Kocha Singida FG

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa Singida Fountain Gate, Ernst Middendorp amesema hajajizuru kuifundisha timu hiyo  kupitia mahojiano aliyofanya na kituo cha Habari cha 947 Joburg kutoka Afrika Kusini ambapo pia  amethibitisha kuwa bado hajaiandikia Singida Fountain Gate barua ya kujiuzulu wadhifa wake kama kocha mkuu wa klabu hiyo.

Kocha huyo amezua sakata kutokana na kudaiwa kutoonekana nchini baada ya kukorofishana na waajiri wake hao kuhusu namna ya kupanga kikosi wakati wa kujadili ripoti ya mchezo dhidi ya Future Fc ya nchini Misri ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi wa 1-0.

Taarifa za ndani zinadai kuwa kocha huyo alichukizwa na maswali kutoka kwa mabosi wa juu wa klabu hiyo hasa yale ya kiufundi ambapo aliamua kuondoka katika kikao hicho.

banner

Kocha huyo tayari yupo nchini Afrika ya kusini ambapo amefanya mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini humo ambapo alisema kuwa ameondoka klabuni hapo baada ya kuona anaingiliwa majukumu yake japo bado hajaandika barua ya kujiuzuru nafasi hiyo.

“Sijali wengine wanafikiria nini nataka kufanya kazi kama kocha na najua ni nini nafanya, napokea message nyingi kutoka kwa wachezaji na hii inaonyesha kujali na ninajivunia hilo”.Alisema kocha huyo mwenye asili ya ujerumani

“Niliona huko baadaye nitakuja kuambiwa sio golikipa huyu mchezeshe huyu, sio beki huyu mchezeshe mwingine, sio hawa viungo wawili wachezeshe hawa wawili hiki ni kitu ambacho nilikiona kitakuja kutokea baadaye na hiyo haifanyiki kwangu, mimi siwezi.

“Waziri wa Fedha, Mmiliki wa Klabu, Mwenyekiti wa Klabu na Menejimenti wote hawapo kwenye uwanja wa mazoezi, hawaoni wachezaji wakifanya kazi hawaoni wachezaji wakimudu mchezo, hawana idea ni Mchezaji gani amejiandaa vizuri kwaajili ya mchezo,”.Alimalizia kusema

Singida FG iliamuajiri kocha huyo baada ya kuachana na kocha Hans Van Pluijm kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho hasa katika ligi kuu.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.