Saturday, May 10, 2025
Home Makala Saido,Bocco Bye Bye Simba Sc

Saido,Bocco Bye Bye Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kutangaza kuachana na John Bocco,Klabu ya Simba sc imeendelea kuachana na mastaa mbalimbali waliomaliza mikataba klabuni hapo ambapo leo hii imetangaza kuachana na Saido Ntibanzokiza ambaye mkataba wake umemalizika klabuni hapo.

Simba sc baada ya kukosa ubingwa wa ligi kuu nchini kwa miaka mitatu mfululizo sasa imeamua kufumua kikosi chote sambamba na utawala ambapo sasa imewarudisha Mohamed Dewji,Crescentius Magori huku Salim Abdalah “Try Again” akisalia katika bodi hiyo kama mjumbe huku wakitaka kurejesha heshima ya klabu hiyo kwa kusajili majembe mapya.

Mabadiliko hayo katika ngazi ya utawala yamewapa nguvu mabosi wa klabu hiyo kufumua kikosi hicho na sasa baada ya John Bocco ambaye amehamishiwa kuwa kocha wa kikosi cha vijana cha klabu hiyo huku Saido akiachwa ili kutoa nafasi za kusajili damu changa kikosini humo hasa kutoka nje ya nchi.

banner

Kuachwa wa mkongwe huyo aliyejiunga na Simba sc akitokea Geita katika msimu wa usajili wa dirisha dogo la Januari mwaka 2023 ambapo msimu huu staa huyo amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa klabu hiyo akifunga mabao 10 katika ligi kuu ya Nbc nchini.

Tayari Mo Dewji ameahidi kufanya usajili wa maana wa mastaa mbalimbali huku akifanikiwa kumshawisha Cletous Chama kusalia klabuni hapo baada ya kukubali kutekeleza yale aliyohitaji katika mkataba wake.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.