Friday, May 9, 2025
Home Makala Pacome Aibua Utata Yanga sc

Pacome Aibua Utata Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Pacome Zouzoua yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya klabuni hapo ambapo amedaiwa kuhitaji dau kubwa la usajili ili kusaini mkataba huo.

Mkataba wa mchezaji huyo unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu ambapo tayari mabosi wa klabu hiyo wameonyesha nia ya kumpa mkataba mpya wa miaka miwili lakini staa huyo anahitaji dau kubwa sambamba na mshahara mkubwa zaidi mara mbili ya huu wa sasa.

Pacome inadaiwa anahitaji mshahara wa zaidi ya shilingi milioni arobaini kwa mwezi mshahara ambao unafanana na anaolipwa staa wa klabu hiyo Stephan Aziz Ki au Cletous Chama ambao ndio wanaongoza kwa mishahara klabuni hapo.

banner

Mpaka sasa bado mazungumzo yanaendelea na mabosi wa klabu hiyo wanaamini kuwa dili hilo litafikia mauafaka mapema kabla staa huyo hajabakisha miezi sita katika mkataba wake wa sasa ili kuepuka kumkosa.

Hata kambi ya mchezaji huyo inaamini ni bora mteja wake huyo asalie Yanga sc kutokana na utulivu alionao sambamba na kupata nafasi ya kucheza chini ya kocha Miguel Gamondi.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.