Klabu ya Yanga sc itawakosa wachezaji wake sita kuelekea katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaofanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa kutokana na sababu mbalimbali.
Farid Musa,Carlos Carlinhos,Haruna Niyonzima,Balama Mapinduzi wote wakisumbuliwa na majeruhi mbalimbali pamoja na kukosa utimamu wa mwili kuelekea mchezo huo huku Abdalla Shaibu Ninja na Yassin Mustapha nao wakiwa wanamalizia matibabu yao ya mwisho.
Tayari kikosi cha Yanga sc kimeondoka jijini Dar es salaam na kuweka kambi katika mkoa wa Mtwara kujiandaa na mchezo huo mkali wakijiandaa kutua Ruangwa siku ya Ijumaa.