Saturday, May 10, 2025
Home Soka Ni Yanga vs Kariobang Sharks Wiki ya Mwananchi

Ni Yanga vs Kariobang Sharks Wiki ya Mwananchi

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imethibitisha kuwa itavaana na Kariobang Sharks ya Kenya katika siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi katika uwanja wa taifa Agosti 4 jijini Dar es salaam.

Awali Yanga ilitangaza kuwaleta klabu ya As Vita kutoka Kongo lakini kutolewa ghafla kwa ratiba ya michuano ya kimataifa ya ligi ya mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kumewafanya Wakongo hao kushindwa kuja nchini kutokana na kubanwa na ratiba.

Pia klabu hiyo ambayo ni mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu nchini wakichukua mara 27 wametangaza viingilio katika mchezo huo ambapo kiingilio cha juu ni shilingi elfu 30 huku cha chini ikiwa ni shilingi elfu 5 katika majukwaa ya viti vya bluu na rangi ya machungwa(orange).

banner

Yanga itabidi walipize kisasi katika mechi hiyo baada ya kufungwa na Sharks katika michuano ya Sportspesa iliyofanyika nchini baada ya kufungwa kwa mabao 2-1 hapo hapo katika uwanja wa taifa.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.