Klabu ya Namungo Fc imekubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Yanga sc katika mchezo wa kombe la mapinduzi uliofanyika katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar.
Bao pekee la faulo lililofungwa na Zawadi Mauya aliyepokea pasi kutoka kwa Haruna Niyonzima lilitosha kupeleka kilio mpaka mkoani Mtwara yalipo makazi ya klabu hiyo.
Namungo Fc sasa itavaana na Jamhuri ambao walitoka suluhu na Yanga sc ili kuamua washindi wa kuingia hatua inayofuata.