Wednesday, May 7, 2025
Home Soka Maxi Apewa Ndinga Mpya

Maxi Apewa Ndinga Mpya

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Maxi Nzengeli amekabidhiwa gari mpya aina ya Toyota Crown na mabosi wa klabu hiyo baada ya kufanya maboresho ya mkataba wake klabuni hapo.

Nyota huyo wa zamani wa As Meniema ya nchini Congo DRC alijiunga na Yanga sc msimu huu ambapo amekua moto wa kuotea mbali akitumika katika nafasi ya kiungo mshambuliaji wa kati ama pembeni kulia na kushoto huku kasi yake na utulivu wake ukimpa nafasi zaidi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Zawadi ya gari hilo ni moja ya vipengele katika mkataba wa staa huyo ambaye katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Big Stars alifanikiwa kufunga mabao mawili na kufikisha jumla mabao matano na asisti mbili katika ligi kuu mpaka sasa huku akitarajiwa kuwasha moto katika mchezo ujao dhidi ya Simba sc novemba 5.

banner

“Huu ni mchezo mkubwa unaotazamwa sana hivyo kila mchezaji anapaswa kuonyesha juhudi na morali ili kufanikiwa katika mechi hiyo yenye ushindani mkubwa”Alisema Maxi akiuzungumzia mchezo huo muhimu kabisa dhidi ya Simba sc.

Maxi ambaye anasifika kwa nidhamu kikosini humo amefanikiwa kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha kocha Miguel Gamondi kutokana na kuwa na maarifa,nguvu pamoja na juhudi binafsi mazoezini na wakati wa mechi.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.