Klabu ya Yanga sc imeamua kuwashirikisha wachezaji 6 wapya itakaowatangaza kuwasajili katika kikosi kipya cha klabu hiyo kitakachoshiriki michuano ya Kagame Cup itkayofanyika nchini mapema mwezi Augusti mwaka huu.
Katika kikosi hicho kipya mastaa wa kikosi cha kwanza wamepewa mapumziko ispokua baadhi ya mastaa wakiwemo Juma Mahadhi,Balama Mapinduzi,Yassin Mustapha,Abdala shaibu,Ramadhani Kabwili na Paulo Godfrey watashiriki huku vijana 10 kutoka timu B nao wakija kuongeza nguvu.
Mastaa wapya waliosajili klabuni hapo wanatajwa kuwa na Djuma Shabani,Ibrahim Ajibu,Herritier Makambo na Fiston Mayele.