Sasa ni rasmi kuwa beki wa klabu ya Simba sc Shomari Kapombe ataukosa mchezo wa Julai 12 baina ya watani wa jadi Simba na Yanga kuwania hatua ya kuingia fainali ya kombe la Shirikisho.
Kwa mujibu wa taarifa kwa Kocha mkuu wa Klabu ya Simba SC, Sven Vanderbroeck Beki huyo wa Kulia wa Klabu hiyo ataukosa mchezo wa nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Asfc) dhidi ya Yanga SC kutokana na kukutwa na jeraha la goti ambalo litamuweka kitandani kwa wiki nne.
Kapombe aliumia katika mchezo wa robo fainali kombe la shirikisho dhidi ya Azam fc ambapo aliumizwa dakika za mwisho baada ya Frank Domayo kumchezea rafu.