Friday, May 9, 2025
Home Soka Depay,Haaland wapiga Hat-tricks kufuzu Qatar 2022

Depay,Haaland wapiga Hat-tricks kufuzu Qatar 2022

by Sports Leo
0 comments

Washambuliaji wa Uholanzi na Norway Memphis Depay na Erling Haaland wamezifungia timu zao za taifa mabao matatu kila mmoja na kuziweka katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya kombe la dunia Qatar 2022 upande wa Bara la Ulaya.

Memphis aliifungia Uholanzi hat trick wakati timu ya taifa ikiishindilia Uturuki mabao 6-1,wakati Haaland yeye akiifungia Norway hat trick katika mchezo ambao uliishudia Norway ikishinda mabao 5-1 dhidi ya Gilbratar katika michezo ya kundi G.

Timu zote hizo mbili zina pointi 13 kila moja kwenye msimamo wa kundi G ambao unahusisha timu nyingine za Uturuki,Montenegro,Latvia na Gilbratar.

banner

Washambuliaji hao wapo katika muendelezo wa viwango vizuri kwa timu zao za taifa na vilabu vyao katika upachikaji mabao.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.