Connect with us

Makala

Dar Derby,Hakuna Kisingizio Kesho

Kesho ndio siku kubwa iliyokua ikisubiriwa na wapenzi wa soka nchini ambapo mchezo baina ya wababe wa soka nchini Simba sc na Yanga sc watavaana katika mchezo wa duru la kwanza wa ligi kuu ya Nbc nchini utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mapema hii leo makocha wa timu hizo walikutana na waandishi wa habari na kuelezea mikakati yao kuelekea mchezo huo wa kesho ambapo kocha Fadlu Davis wa klabu Simba sc alieleza mikakati yake akikiri ubora wa Yanga sc.

“YangaSC wasingeshinda ligi mara tatu mfululizo kama hawakuwa timu nzuri, ni timu ambayo imekuwa pamoja kwa miaka mitatu sasa na wameshinda ligi mara tatu.”Alisema Fadlu Davis ambaye ni Raia wa Afrika ya kusini.

“Ingawa tunawaheshimu,tumewachambua kwa kina, tunajua kabisa jinsi wanavyokusudia kukabiliana na mchezo.Tumeshachambua mechi zao zote hadi sasa.”aliendelea kusema kwa msisitizo

“Ni timu bora tu itakayoshinda siku hiyo. Tunapaswa kuzingatia mpango wetu.Tunapaswa kuzingatia mkakati wetu.”Alimalizia kocha huyo anayependa kushambulia kuanzia nyuma ambapo mabeki wanakua wanashiriki kwa kiasi kikubwa kupandisha mashambulizi.

Naye kocha mkuu wa klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi alisema kuwa haweza kuahidi idadi ya magoli lakini wamejipanga kwa mbinu kali zaidi ili kuibuka na ushindi.

“Tuna furaha kubwa kuelekea kwenye ligi huku tukiwa na mchezo muhimu wa Derby.Tupo vizuri, tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri hapo kesho. Hatujabadilika sana kwenye maandalizi tumejiandaa kama ambavyo tumekuwa tukifanya hapo awali”.alisema Gamondi anayependa kutumia viungo wengi katikati ya uwanja.

“Tumetokea kwenye wiki ya FIFA na mara nyingi tunapata changamoto kidogo ya maandalizi kwani wachezaji wetu wengi wanakuwa kwenye majukumu ya timu za TAIFA. Kwa mfano kuna wachezaji wamefika jana na wengine wanaingia leo kwa mantiki hiyo lazima upate ugumu kwenye maandalizi lakini tutafanya kila liwezekanalo”.aliendelea kusema kocha huyo raia wa Argentina.

“Tunawaheshimu wapinzani wote tunaocheza nao ligi kuu. Ni kweli kesho tuna mechi ngumu kwani ni Derby, lakini tunajua namna tunauendea mchezo. Kila mara nasema mimi huwa sitazami sana historia. Yaliyopita yamepita, malengo yetu ni kutazama yanayokuja mbele yetu.” alimalizia kusema Miguel Gamondi ambaye mwishoni mwa msimu huu atakua huru baada ya kumaliza mkataba katika klabu hiyo.

Mpaka sasa timu hizo kila moja haijafungwa mchezo wowote katika ligi kuu bara ambapo Simba sc imecheza michezo mitano ikiwa na alama 13 huku Yanga sc ikicheza michezo minne ikiwa na alama 12.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala