Friday, May 9, 2025
Home Soka Corona Yamkwamisha Ighalo

Corona Yamkwamisha Ighalo

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo atakosa mazoezi na klabu hiyo nchini Uhispania kutokana na hofu kwamba virusi vya corona vinaweza kumzuia kuruhusiwa kuingia nchini Uingereza .

Ighalo mwenye umri wa miaka 30, alisafiri kuelekea mjini Manchester kutoka China wikendi iliopita baada ya kutia saini kandarasi ya mkopo kutoka klabu ya Shenghai Shenhua.

”Angependelea kujiunga na wachezaji wengine ili kuweza kujuana”, alisema Mkufunzi Ole Gunnar Solskjare akizungumza na runinga ya MUTV.

banner

Wakati huo huo kiungo wa kati wa Man United Scott McTominay na beki Axel Tuanzebe ambao wote wamekuwa na majeraha ya muda mrefu watasafiri kuelekea Uhispania.

United hawatarudi hadi siku ya Ijumaa kabla ya mechi yao ya ligi ya Uingereza dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 17 February.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.