Connect with us

Makala

Kisa Caf,Mechi Nbc Zasogezwa Mbele

Michezo ya ligi kuu ya Nbc kwa timu za Yanga Sc na Simba Sc katika raundi ya 12 imesogezwa mbele ili kutoa nafasi kwa klabu hizo kujiandaa na michuano ya Kimataifa inayotarajiwa kuanza mwezi huu katika hatua ya makundi.

Yanga sc ambayo imepangwa kundi A na timu za Tp Mazembe,Mc Algers na Al Hilal ya Sudan siku ya Novemba 26 ambapo itaanzia nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa huku Simba sc nao wakiwakaribisha Bravo do Maquiz ya Msumbiji siku ya Novemba 28 hapo hapo Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Michezo ya ligi kuu iliyoahirishwa ni hiyo ambayo Yanga sc alikuwa anacheza dhidi ya Fountain Gate FC na Pamba JIJI FC dhidi ya Simba imeondolewa na itapangiwa tarehe nyingine ili kuzipa nafasi timu hizo kujiandaa na michezo ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga sc ambayo inashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Simba sc ambayo nayo inashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo zote zitaanza kuisaka tiketi ya kufuzu robo fainali mwezi huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala