Connect with us

Soka

Chelsea Macho Yote Kwa Kai Havertz

Kocha wa Chelsea  Frank Lampard amewahimiza mabosi kuwa anataka kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Hai Havertz kutoka Bayern Leverkusen katika dirisha lijalo la usajili la  majira ya joto.

Leverkusen hawajapokea ofa rasmi kwa ajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 lakini inaaminika Real Madrid pamoja na Bayern Munchen wameshafanya mazungumzo na klabu hiyo huku awali ilidaiwa kuwa Chelsea ipo mbioni kumsaini lakini inaonekana bado dili bichi.

Mpaka sasa Havertz  ameshafunga magoli 11 na Assist 5 katika mechi 26 za Ligi Kuu ya Ujerumani msimu huu huku mkataba wake na Leverkusen ukifikia tamati 30 Juni, 2022.

Inasemekana bosi wa Chelsea Roman Abramovich yuko tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa kumsajili kinda huyo baada ya kukubaliana na klabu ya Rb Leipzig juu ya mshambuliaji Timo Werner.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka