Connect with us

Soka

Breaking News..Simba Waliamsha Dude Usajili

Klabu ya Simba Sc imeendelea kuonyesha umwamba katika dirisha la usajili baada leo hii kutangaza usajili wa kiungo hatari kutoka katika klabu Al Hilal ya Sudan anayeitwa Sharaf Eldin Shiboub kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kiungo huyo mrefu ni mchezaji bora wa nafasi ya kiungo mara mbili katika ligi kuu ya nchini humo ana umri wa miaka 26 ambao ameutimiza mwezi huu wa sita huku akiwa amefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Sudan mara nne tofautitofauti.

Shiboub amesajiliwa simba ili kuongeza nguvu katika safu ya kiungo ya timu hiyo iliyoshiriki ligi ya mabingwa barani Afrika na kutolewa hatua ya robo fainali japo haijafahamika hadharani kama usajili huo umekuja kuziba nafasi ya Mghana James Kotei ambae mkataba wake umeisha klabuni hapo na mpaka sasa hakuna mazungumzo yaliyofanyika kuhusu kumuongezea hali ambayo inaleta sintofahamu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka