Friday, May 9, 2025
Home Soka Aucho Arejea Yanga sc

Aucho Arejea Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Khalid Aucho amerejea rasmi kikosini baada ya kukosekana katika michezo mitatu baada ya kufungiwa na bodi ya ligi kuu nchini kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union Ibrahim Ajibu mwaka jana Novemba 8 wakati wa mchezo wa ligi kuu baina ya timu hizo uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Aucho amefanikiwa kumaliza adhabu hiyo baada ya kuikosa michezo mitatu dhidi ya Mtibwa Sugar uliofanyika Disemba 16 na ule wa Tabora United uliofanyika Disemba 22 mkoani Dodoma na mchezo wa juzi dhidi ya Hausing Fc wa kuwania kufuzu 32 bora ya kombe la Shirikisho.

Kocha Gamondi amefurahishwa na urejeo wa kiungo huyo ambaye anampa machaguo mengi katika eneo la kiungo kutokana na umuhimu wake katika kukaba na kuanzisha mashambulizi kwa ufanisi zaidi kuliko viungo wengine klabuni humo.

banner

Yanga sc itacheza na Kagera Sugar hapo kesho katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera saa kumi jioni ambapo mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wa alama tatu kwa timu zote.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.