Home Makala Yanga Sc Yazindua Jezi za CCL

Yanga Sc Yazindua Jezi za CCL

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imezindua jezi maalumu ambazo itazitumia katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika hatua ya makundi ambapo itaanza mchezo huo siku ya ijumaa dhidi ya CR Belouzdad ya nchini Algeria.

Katika jezi hizo zilizozinduliwa mapema jioni ya leo kuna aina tatu za nyumbani,ugenini na jezi ya tatu ambayo itatumika pale tu hizi mbili zinapoingiliana rangi na timu pinzani katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Jezi hizo mpya zilizozinduliwa zimebuniwa na mbunifu Sharia Ngowi ambapo zimekua na maana mbalimbali  kama zilivyo jezi mpya za nyumbani za Yanga sc za Ligi ya mabingwa Afrika 2023/24 yameandikwa majina ya wachezaji walioiwezesha timu hiyo kufuzu hatua makundi ya michuano hiyo baada ya miaka 25 pamoja na nchi wanazotoka.

banner

Katika jezi ya Dark Blue (Third Kit) zimeandikwa sehemu mbalimbali za vivutio vya utalii Tanzania kama vile mbuga za Wanyama na sehemu za kumbukumbu za kihistoria.

Tayari klabu hiyo imetangaza kwamba jezi hizo zitauzwa kwa bei ya shilingi elfu hamsini kwa reja reja na kutakua na matoleo machache kama mwaka jana ambapo walizalisha jezi elfu hamsini pekee.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.