Connect with us

Makala

Yanga sc Yaipiga Kaizer Chiefs

Ikiwa ni kilele cha wiki ya mwananchi,klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Yanga sc katika mchezo huo ilitumia vikosi viwili kwa kila kipindi huku pia ikiwatambulisha rasmi baadhi ya mastaa wake akiwemo Jonas Mkude,Maxi Nzengeli pamoja na Gift Fred huku pia Pacome Zouzou na Kouassi Attohoula Yao waliongia kipindi cha pili.

Beki na nahodha wa Yanga sc Bakari Mwamnyeto akiwa katika harakati za kufunga goli kutokana na mpira wa kona.

Bao pekee la Yanga sc katika mchezo huo lilifungwa na Kennedy Musonda ambaye alipokea pasi ya Maxi Nzengeli na kufanikiwa kumzidi maarifa kipa Itumeleng Khune dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Yanga sc walikuja na kikosi kipya huku wachezaji kama Djigui Diarra,Aziz Ki na Khalid Aucho wakianzia benchi kutokana na kutokufanya maandalizi ya kutosha mazoezi baada ya kuchelewa kuwasili nchini.

Tamasha hilo hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa nane ikiwa ni maalumu kwa ajili ya utambulisho wa mastaa wapya wa kikosi hiko ambapo lilitanguliwa na burudani za kutosha za wasanii na madj wa kisasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala