Friday, May 9, 2025
Home Makala Yanga Sc Kukomaa na Feisal

Yanga Sc Kukomaa na Feisal

by Sports Leo
0 comments

Inaelezwa kuwa klabu ya Yanga sc  ipo mbioni kufanya mazungumzo na kiungo wa Azam Fc ,Feisal Salum ili arejee kwenye kikosi chao kwa mara nyingine mara baada ya kuondoka Kwa miamba hiyo ya Kariakoo msimu Wa 2022/23.

Mabosi wa Yanga sc wanamhitaji Feisal kwenye kikosi chao Kwa udi na uvumba ili akazibe pengo la kiungo wao Stephen Aziz Ki Ambaye huenda akatimkia katika klabu ya Wydad Casablanca ya Nchini Morocco Mwishoni mwa Msimu huu.

banner

Feisal tangu ajiunge na Azam Fc amekua nguzo ya timu hiyo kwa misimu miwili sasa na mabosi wa Yanga sc wanaona ni wakati sahihi wa kumrudisha klabuni hapo kwa mara nyingine baada ya kupata ofa ya pesa ndefu kutoka Wydad Athletic Club ya kumuuza Aziz Ki.

Mbali na ofa ya Aziz Ki pia klabu hiyo itapata pesa nyingi kwenye mauzo ya Clement Mzize anayewania na klabu ya Al Ahly Tripoli ya Libya pamoja na Djigui Diarra ambaye nae kuna ofa mbili nzito mezani.

Mpaka sasa inasemekana Feisal yuko tayari kurudi Jangwani kutokana na mzigo mzito ambao Yanga sc wameuweka mezani huku kikwazo ikiwa ni mama yake mzazi ambaye hataki mwanae arudi klabuni hapo.

Mabosi wa Yanga sc wenyewe wapo tayari kuongea na mama wa mchezaji huyo ili kumaliza mgogoro uliotokea kipindi hicho ili atoe baraka kwa mwanae kurudi klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.