Connect with us

Makala

Tottenham Wagoma kumuuza Eriksen

Mchezaji wa Tottenham Christian Eriksen agomewa kuuzwa na uongozi wake katika timu ya Inter Milan kwa dau la pauni milioni 10 ambalo liliwekwa mezani na mabosi hao ili kupata saini ya mchezaji huyo.

Christian Eriksen mkataba wake unakaribia kufikia ukingoni lakini mabosi wa Tottenham hawajapata presha kwani wamekomaa na wanahitaji mara mbili ya dau hilo yaani pauni milioni 20 ndipo Inter Milan wafikiriwe kumpata nyota huyo.

Kocha wa Tottenham Jose Morurinho amesema kuwa endapo mchezaji huyo ataachiwa na kuwa mchezaji huru Eriksen alishawahi kumuambia matamanio yake ni kucheza ndani ya Real Madril na Barcelona hivyo lengo lake litakamilika  kwani anajiamini kuwa ni mchezaji bora.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala