Connect with us

Makala

Singida Black Stars Yapoteza kwa Kmc

Klabu ya Singida Black Stars leo imekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Kmc katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Kmc ikiwa nyumbani chini ya kocha Kally Ongara imebahatika kupata mabao hayo kipindi cha kwanza dakika za 35 na 40 yakifungwa na Oscar Paul aliyekua mwiba mchungu kwa Black Stars.

 

Oscar alifunga bao la kwanza kutokana na kutumia vyema makosa ya mlinzi wa Singida Black Stars Anthony Bi Tra Bi aliyeshindwa kuokoa mpira uliokua unazagaa.

Bao la pili la lilitokana na pasi nzuri ya Daruweshi Saliboko aliyempasia vyema mfungaji na kumchambua golikipa wa Singida Black Stars Hussein Salum Masalanga.

Singida Black Stars hawakua na bahati baada ya Elvis Rupia kukosa penati dakika ya 48 ya mchezo kutokana na Augustine Sowah kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Mpaka dakika 90 zinakamilika wenyeji Kmc walifanikiwa kuchukua alama zote tatu na kufikisha alama 22 katika michezo 18 ya ligi kuu wakisimama katika nafasi ya sita ya msimamo.

Singida Black Stars wenyewe wameendelea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama 34 katika michezo 18 ya ligi kuu ya Nbc nchini.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala