Mshambuliaji wa Azam Fc, Andrew Simchimba ambaye alikuwa kwenye hesabu za mabosi wa Simba Sc waliokuwa wanahitaji saini yake msimu wa dirisha dogo na dili lao kutibuliwa amejifunga ndani ya klabu ya Azam kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Nyota huyo aliyekuwa anakipiga Coastal Union hapo awali na kurejea Azam Fc mkataba wake ulikuwa umalizike mwaka huu mwezi Septemba lakini ameongezewa kandarasi ya miaka mitatu ambapo atadumu hapo hadi 2023.
Uongozi wa Azam Fc umekuwa unamuamini Simchimba kwani amekuwa akitimiza majukumu yake kwenye timu hiyo kama ipasavyo.