Connect with us

Makala

Simba Sc Yatinga Nusu Fainali Caf

Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga klabu ya Al Masry kwa chamoto ya mikwaju ya penati 4-1 baada ya sare ya 2-2 katika michezo yote miwili.

Katika mchezo kwa kwanza ugenini nchini Misri Simba sc ilikubali kufungwa mabao 2-0 lakini katika mchezo wa leo mpaka kufikia kipindi cha kwanza tayari ilikua imesawazisha mabao hayo.

Kocha Fadlu Davis aliamua kuanza na mshambuliaji Steven Mkwala akiamuacha nje Lionel Ateba na hatimaye mabadiliko hayo yalilipa baada ya Ellie Mpanzu kufunga bao la kwanza kwa shuti kali dakika ya 22 akiwachekecha mabeki wa Al Masry na kufunga.

Mukwala nae aliunganisha kwa ustadi krosi ya Mohamed Hussein na kuandika bao la pili kwa kichwa dakika ya 32 ya mchezo huo uliokua mkali na wa kusisimua huku wingi wa mashabiki ukichagiza ubora wa mchezo huo.

Kipindi cha kwanza Simba sc iliokwenda ikiwa na matokeo ya 2-0 lakini hali haikua shwari kipindi cha pili baada ya timu hiyo kukosa nafasi kadhaa huku waarabu wakipoteza muda mwingi kwa kujiangusha mara kwa mara.

Mwamuzi wa mchezo huo licha ya kuongeza dakika 10 lakini matokeo hayakubadilika na mpaka filimbi ya mwisho matokeo yalikua 2-0 na kuufanya kuwa sare ya 2-2 kwa ujumla na ndipo ilipoamuriwa mikwaju mitano ya penati kwa kila timu.

Kipa Moussa Camara ndie shujaa wa Simba sc baada ya kucheza mikwaju miwili ya penati huku Shomari Kapombe naye akiibuka shujaa baada ya kufunga penati ya mwisho ya ushindi na kuivusha Simba sc hatua ya nusu fainali.

Simba sc sasa itakutana na   Fc Stelleboch ya Afrika kusini katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya kombe la shirikisho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala