Simba sc imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika huku ikiongoza kundi A baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya As Vita kwa mabao 4-1 katika mchezo uliomalizika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Mabao ya Simba sc katika mchezo huo yalifungwa na Cletous Chama,Luis Miqquissone,Larry Bwalya na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo huku walikua wakihitaji alama moja kufuzu hatua ya robo fainali.