Connect with us

Makala

Sakho Awashtua Caf

Bao lililofungwa na Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Pape Osmane Sakho dhidi ya klabu ya Rs Berkanee limechaguliwa kuwa bao bora la wiki katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Sakho alifunga bao hilo kwa ustadi mkubwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam akipokea mpira katika kona ya eneo la box na kuingia nao mpaka ndani ya boxi akiwalaghai mabeki kama anataka kupiga huku akisogea zaidi na kufunga kwa shuti kali la chini chini lililomshinda kipa na kuandikia Simba sc bao lililodumu mpaka mwisho wa mchezo huo na kuipa alama tatu muhimu.

Simba sc ilikusanya alama tatu katika mchezo huo na kukaa kileleni mwa kundi huku Berkane na Asec Mimosa wakiwa katika nafasi ya pili na tatu kwa alama 6 huku Gendamarie wakiwa mkiani na michezo ijayo Simba sc itasafiri mpaka nchini Ghana kuwavaa Mimosa na Berkane watawavaa Us Gendamarie kuhakikisha wanafuzu hatua ya robo fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala