Connect with us

Makala

Saido Hashikiki Geita Gold sc

Kiwango maridhawa kilichoonyeshwa na nyota wa zamani wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza kimewakosha wadau mbalimbali wa michezo nchini ambapo mpaka sasa amekua msaada katika klabu yake ya Geita Gold Sc akiisaidia kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Prisons Fc.

Saido katika mchezo huo alitoa pasi mbili za mabao huku mpira wake uliookolewa na beki ukisababisha moja ya mabao ya klabu yake ambapo alitoa pasi za mabao kwa Danny Lyanga na Edmund John na kufikisha jumla ya assisti nne katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu.

Saido aliachana na Yanga sc ambapo alimua kujiunga na Geita Gold sc lakini licha ya timu hiyo kuwa changa haijamzuia kufanya vizuri katika ligi kuu msimu huu ambapo mpaka sasa klabu hiyo iko katika nafasi ya sita ikiwa na alama 17 katika michezo 12 ya ligi kuu nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala