Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amerejea katika mazoezi baada ya kuwa nje kutokana na kupata maambukizi ya virusi vya Corona.
Pogba ana uwezekano mkubwa wa kutocheza mchezo wa kwanza ndani ya Premier Septemba 19 ambapo klabu yake ya Man United itavaana na Crystal Palace kwenye uwanja wa Old Trafford.
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa,kurejea kwa Pogba kwenye mazoezi hakumpi asilimia 100 kuwa atashiriki mechi ya kwanza kwani hayupo kwenye sehemu ya kikosi ambacho kinaendelea na mazoezi.