Man United Waitaka Saini Ya Bale

0

Manchester United imeingia kwenye rada ya kumnasa nyota wa Real Madrid, Gareth Bale ili ajiunge na kikosi hicho kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21 kabla dirisha la usajili halijafungwa Octoba 5.

Kocha mkuu wa klabu hiyo,Ole Gunnar Solskjaer ameamua kumvuta Bale ndani ya United baada ya kupoteza matumaini ya kuipata saini ya Jadon Sancho wa Borussia Dortmund.

Bale akiwa ndani ya Real Madrid tangu msimu wa 2013, amecheza jumla ya mechi 171 na kupachika mabao 80 akitokea klabu ya Tottenham Hotspurs ambayo inashiriki ligi kuu England.

Leave A Reply

Your email address will not be published.