Friday, May 9, 2025
Home Makala Neema Yamshukia Bacca

Neema Yamshukia Bacca

by Sports Leo
0 comments

Rais wa klabu ya Yanga sc Eng.Hersi Said ametangaza neema kwa beki wa klabu hiyo Ibrahim Hamad Bacca kwa kuamua kumuongezea mkataba mpya sambamba na maboresho makubwa ya mshahara wake klabuni hapo.

Hersi amesema hayo akiwa njiani kurejea nchini kutoka nchini Nigeria ambapo amefanikiwa kuongoza Yanga sc kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Rivers United mchezo ambao beki huyo alicheza akionyesha kiwango kikubwa zaidi.

Bacca ameingia katika msimu wake wa pili tangu asajiliwe na klabu ya Yanga sc januari mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kmkm ya mjini Unguja hasa baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya kombe la mapinduzi mwaka jana.

banner

Mchezaji huyo kwa siku za karibuni amekua jibu zuri la tatizo la Yanga sc la kufungwa mipira iliyokufa kwa vichwa ama mipira ya kutenga ambapo beki huyo amekua na uwiano mzuri wa kuokoa hatari hizo.

Hersi ametambua mchangowa Bacca na kuamua kufichua kuwa tayari mazungumzo yameanza kwa ajili ya mkataba mpya kwa beki huyo sambamba na maboresho ya stahiki zake muhimu.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.