Bondia wa Kimataifa Hassan Mwakinyo ameendeleza ubabe kwa kumtwanga Bondia Katemba Kuvesa kutoka nchini Afrika Kusini, katika pambano lisilo la Ubingwa lililoandaliwa kwa ajili ya kupata fedha za kununua taulo za kike lililofanyika Aprili 23, 2024 Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ambaye alikua mgeni rasmi katika pambano hilo amempongeza Bondia Mwakinyo kwa ushindi huo na kuzidi kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa
Pambano hilo limeandaliwa na Mkurugenzi wa Lady in Red Mhe.Sophia Mwakagenda likiwa na lengo la kukusanya fedha za kusaidia ununuzi wa taulo za kike ambapo pia kulikua na mapambano ya awali yaliyojumuisha wabunge.