Beki wa Bilioni Moja Kutua Simba sc

0

Katika kujiweka sawa kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika klabu ya Simba sc inaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa timu ya taifa ya Burundi anayecheza katika klabu ya Chipa United ya nchini Afrika ya Kusini Frederic Nsabiyumva.

Beki huyo ambaye kwa mujibu wa klabu yake bei yake ni shilingi milioni 958 za kitanzania ambazo timu hiyo inatakiwa kulipwa ili kumuachia beki huyo kwa mujibu wa wakala wake Herve Tra Bi ambaye ni Raia wa Afrika ya Kusini.

Simba sc inahitaji beki mpya wa kati mwenye kasi kusaidiana na Pascal Wawa na Joash Onyango ambao wana kasi ndogo hivyo beki Mrundi mwenye miaka 25 anaonekana kuwa chaguo sahihi kwa kocha Sven Vandebroek.

Leave A Reply

Your email address will not be published.