Connect with us

Makala

MVP Atua Yanga sc

Klabu ya Yanga sc imemtambulisha kiungo wao mpya raia wa Ivory Coast Pacome Zouazoua ambaye amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili kuja kusaidia mwendelezo wa kunyakua makombe klabuni hapo.

Kiungo huyo mshambuliaji ndie mchezaji bora wa ligi kuu ya soka ya Ivory Coast akiitumikia klabu ya Asec Mimosas ambapo alifunga mabao saba na kusaidia upatikanaji wa mabao mengine manne katika ligi kuu ya nchini humo.

Pacome anaungana na Stephane Aziz Ki na Koausi Yao ambao wametokea pamoja katika klabu hiyo ya Asec Mimosas ya nchini humo.

Kiungo huyo ana uwezo wa kucheza vyema nafasi ya kiungo mshambuliaji na mkabaji ambapo kusajiliwa kwake kunatajwa kuwa anachukua nafasi ya kiungo Yannick Bangala ambaye nae tayari yupo katika harakati za kuondoka klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala