Connect with us

Makala

Msuva Matatani Cas

Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco imepeleka malalamiko yake FIFA kwenye idara ya usuluhishi wa kesi za michezo (Cas)juu ya mchezaji wao raia wa Tanzania, Simon Msuva kwa kukiuka vigezo na masharti vilivyopo kwenye mkataba wake.
Wydad wanadai kuwa wamemlipa stahiki zake za kifedha tangu Mei mwaka jana lakini mchezaji huyo alidanganya umma na kuondoka klabuni hapo bila kumjulisha mtu yeyote huku akifahamu kwamba ana mkataba na klabu hiyo na anatakiwa kukaa klabuni hapo.
Wydad wanamtaka Msuva kulipa faini ya Dola za Kimarekani 500,000 huku pia kwa upande wa mchezaji naye alishapeleka malalamiko yake katika mahakama hiyo kutokana na kuwadai klabu hiyo kiasi kikubwa cha pesa ya usajili na mishahara yake ambayo hajalipwa kwa kipindi fulani tangu ajiunge akitokea Difaa El-Jadid.
Msuva yupo nchini akisubiri uamuzi wa mahakama hiyo ambapo kwa kipindi hiki amekua akijifua na timu ya akademi ya Cambiasso iliyopo jijini Dar es salaam huku akisubiri hatma ya kesi hiyo kutokana na jinsi ikiamuliwa na mahakama hiyo kubwa na yenye mamlaka ya mwisho katika uamuzi wa kesi za michezo duniani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala