Katibu mkuu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni Mh.Gerson Msigwa Februari 23 amewakabidhi klabu ya Simba Sc kiasi cha shilingi 10 ikiwa ni zawadi ya goli la mama kama ulivyo utaratibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan hufanya kila timu inapofunga magoli na kushinda mechi za kimataifa.
Fedha zimekabidhiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo klabu hiyo ilikua katika mazoezi ya jioni kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc utakaofanyika uwanjani hapo Februari 24 2024.
Msigwa amekabidhi fedha hizo ikiwa ni za ushindi wa magoli 2-0 ilioupata Simba dhidi ya CS Constantine katika mechi ya mwisho ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.
Simba sc iliifunga Sc Constantine ya nchini Algeria katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya kundi A la kombe la Shirikisho na kuifanya Simba sc kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Simba sc bado ina nafasi ya kupokea kiasi kingpins endapo itashinda katika mchezo dhidi ya Al Masry katika hatua ya robo fainali ambapo ikiwa ni matarajio ya wengi kuwa itafanya vizuri.