Connect with us

Makala

Ligi Raundi Ya Sita Inaanza Hivi

Ligi kuu Tanzania Bara raundi ya sita inaendelea leo Octoba 14,ambapo timu nane zitavaana katika viwanja vinne tofauti kwaajili ya kusaka pointi tatu muhimu.

Raundi ya tano ilimalizika na kuwaacha Azam Fc wakiwa ni vinara kwa pointi 15 huku Simba Sc wakishika namba 2 na pointi 13 sawa na Yanga sc ambao wameshika nafasi ya tatu kwa mpishano wa mabao.

Leo katika raundi ya sita,Biashara United itawakaribisha Ihefu Fc uwanja wa Karume majira ya saa 10:00 jioni huku JKT Tanzania ikivaana na Ruvu Shooting saa 8:00 mchana katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

KMC ambao ni vijana wa Kinondoni itawakaribisha Coastal Union uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni huku Namungo Fc ikipambana dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Majaliwa majira ya saa 10:00 jioni.a

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala