Simba Sc inatarajiwa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo fc siku ya Jumapili Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote kupambania taji hilo muhimu kwani timu itakayo shinda na kunyakua kombe ndiyo itakayo iwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho.
Patrick Rweyemamu amabaye ni meneja wa Simba amesema kuwa kikosi ambacho kilikwenda Tanga kucheza na Coastal Union kisha kikamalizana na Polisi Tanzania kule Moshi ndicho ambacho kitaelekea Sumbawanga.
Wachezaji ambao walikosa michezo hiyo miwili na inatarajiwa watakosa fainali ni Ibrahim Ajib, Sharaf Shiboub, Rashid Juma, Haruna Shamte, Shiza Kichuya, Cyprian Kipenye na Tairone Santos.