Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga sc Cedrick Kaze amefafanua suala la mchezaji Benard Morrison kutojumuishwa katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Rivers United ya nchini Nigeria huku taarifa zikidai kuwa hakushiriki mchezo huo baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu akiwa kambini.
Kaze amefafanua suala hilo baada ya kurejea nchini na kikosi hicho wakiwa na mtaji wa mabao mawili waliyoshinda ugenini katika mchezo huo wa hatua ya kwanza uliofanyika nchini humo siku ya jumapili jioni.
“Morrison alipata shida kidogo ya msuli kwenye mazoezi ya mwisho hapa Nigeria, kama benchi la ufundi tukaona sio sawa kumlazimisha acheze kwani anaweza kuumia zaidi”
“Tuliamua kumuondoa kwenye mpango wa mechi ili kumpa nafasi ya kuwa sawa kabisa kwaajili ya mechi zinazofuata,”Alisema Kaze
Nyota huyo ambaye amerudi Yanga msimu huu akitokea Simba amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali, Kaze amesema bado watamtumia kwenye mechi zijazo.