Thursday, May 8, 2025
Home Makala Azam Fc Yachukua Alama 3 Kmc

Azam Fc Yachukua Alama 3 Kmc

by Sports Leo
0 comments

Hatimaye kocha mpya wa klabu ya Azam Fc Rachid Taoussi ameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Klabu ya Kmc katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Kocha Taoussi alianza na mfumo wa kukabia juu ulioisumbua Kmc chini ya Abdihamid Moulin na kufanya Azam Fc ipate bao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Idd Nado aliyepokea pasi nzuri ya Feisal Salum.

Feisal Salum tena alimtengenezea bao la pili Lusajo Mwaikenda baada ya kumpa pasi nzuri ndani ya eneo la hatari na kumtungua kipa wa Kmc.

banner

Nassoro Saiduni alipokea pasi nzuri ya Paschal Msindo na kuwapiga chenga mabeki wa Kmc na kisha kufunga bao tamu dakika ya 60 ya mchezo.

Nathaniel Chilambo alifanya kazi ya juhudi kubwa kuanzisha shambulizi kisha kuwahi kumpa presha beki Fredy Tangaro dakika ya 67 na kumsababisha kujifunga bao lililokua na nne kwa Azam Fc.

Sasa Azam Fc imefikisha alama tano kwa michezo mitatu huku Kmc ikifikisha alama nne katika michezo minne ya ligi kuu nchini huku mchezaji Feisal Salum akiibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.