Friday, May 9, 2025
Home Makala Azam Fc Mbabe wa Kmc

Azam Fc Mbabe wa Kmc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Manispaa ya Kinondoni (Kmc) uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Azam Fc ikianza na kikosi chake cha kila siku kikiwa na mabadiliko machache ambapo Yeison Fuentes alimpisha Edward Charles Manyama eneo la beki ya kati na utatu wa Feisal Salum,Gibril Sillah na Kipre Junior ulitawala eneo la mbele na kufanikiwa kupata bao la kwanza kwa kona safi ambapo Yannick Bangala alifunga kwa kichwa dakika ya 11 ya mchezo.

Bao hilo lilidumu dakika tatu tu baada ya Waziri Junior kufunga bap zuri la kusawazisha dakika ya 15 baada ya kuwazidi maarifa walinzi pamoja na Kipa wa Azam Fc Mustafa Mohammed.

banner

Gibril Sillah alifunga bao la ushindi kwa Azam Fc dakika ya 37 ya mchezo akiwazidi maarifa walinzi wa Kmc.

Baada ya dakika 90 kumalizika Azam Fc waliondoka na alama tatu muhimu zinazowafanya wafikishe alama 60 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc huku Kmc wakiwa nafasi ya sita ya msimamo na alama 33.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.