Klabu ya Mtibwa Sugar imeuhamishia mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Simba sc katika uwanja wa Manungu ulioko mjini Turiani mkoani Morogoro kutoka katika uwanja wa Jamhuri uliopo Morogoro mjini baada ya mamlaka kujiridhisha na ubora wa uwanja huo.
Mara kadhaa mechi ambazo zinawahusisha timu za Simba sc na Yanga sc huchezwa katika uwanja wa Jamhuri kutokana na kuwa idadi kubwa ya mashabiki lakini sasa imekua tofauti baada ya uwanja wa Manungu kuwa tayari kwa michezo ya ligi kuu baada ya kufanyiwa matengenezo.
Uwanja wetu wa Manungu tumeufanyia ukarabati, hivyo mechi yetu na Simba itachezwa uko,”amesema Abubakar Nassor ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Mtibwa sugar ambaye ameongeza kuwa;
“Mashabiki wetu wajiandae kuangalia ama kuisapoti timu yao kwenye uwanja wao, tunategemea watafurahia jambo hilo,”amesema.
Mchezo huo utachezwa Jumamosi januari 22 katika uwanja wa huo ambapo Simba sc watakua na kazi nzito ya kuhakikisha wanaibuka na alama tatu baada ya kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbeya City kwa bao 1.