Mzimbabwe wa Azam Fc,Prince Dube ameweka wazi kuwa ishu kubwa kwake siyo kufunga mabao bali kuwatengenezea wenzake nafasi ya kufunga wakiwa uwanjani.
Streika huyo wa mabao amesema kuwa hakuna maana yoyote ile ya kufunga mabao bali anapambana zaidi kukisaidia kikosi chake kifanye vizuri katika ligi kuu bara.
Dube ndiye kinara wa sasa wa ufungaji katika ligi kuu akiwa na mabao sita akifuatiwa na mchezaji wa Simba Sc,Meddie Kagere mwenye mabao manne huku akishikilia kiatu cha dhahabu cha msimu ulioisha wa 2019/2020.
“Ikitokea nikafunga,nitashukuru lakini hata nisipofunga nitamsaidia mwenzangu yeyote wa kikosi changu afunge ili timu yangu ishinde kama ambavyo wenzangu wananisaidia mimi kufunga katika michezo iliyopita”alisema Dube