Staa wa klabu ya Namungo Reliant Lusajo amesema hana presha endapo akisajiliwa na klabu ya Yanga kutokana na kuamini kiwango chake cha sasa.
Lusajo aliyewahi kusajiliwa Yanga kisha kukosa nafasi chini ya kocha Ernie Brandt kutokana na kutokua na uzoefu ambapo alijiunga na klabu mbalimbali kama Toto Afrika kisha kutua Namungo anakowika mpaka sasa.
“Nina amini kwamba uwezo wa mchezaji huwa haujifichi, iwapo nitapata nafasi ya kurejea Yanga nitaendelea na kasi yangu ya kutupia pale nitakapopata nafasi.
“Uzuri ni kwamba kwa sasa nimezidi kuimarika na kuwa na uwezo wa kufunga jambo ambalo linanifanya niamini kwamba ninaweza kucheza popote ndani na nje ya Bongo,” amesema.