Connect with us

Makala

Gormahia Yatembeza Bakuli

Kama ulijua bakula linatembezwa jangwani pekee basi utakua umechemsha baada ya mfumo huo wa kuomba michango kuiangukia klabu ya Gormahia ya nchini kenya baada ya kutetereka kiuchumi siku za hivi karibuni.

Klabu hiyo imekua na wakati mgumu tangu wadhamini wake kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportspesa kujitoa kudhamini klabu hiyo kutokana na kodi kubwa iliyowekwa katika michezo ya kubahatisha.

Gormahia wanaandaa hafla ya kuchangisha fedha ili kuweza kushiriki mechi ya mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa afrika dhidi ya Us Alger kutoka nchini Algeria mechi ambayo wakishinda wataenda hatua ya makundi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala