Beki Kelvin Yondani ametua katika klabu ya Polisi Tanzania kama mchezaji huru baada ya kuachana na Yanga sc msimu uliopita kutokana na kushindwana katika maslahi.
Beki huyo mkongwe ametua Polisi Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao utaisha rasmi januari mwakani.
Polisi Tanzania itafaidika na uwepo wa mkongwe huyo kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha kucheza ligi kuu nchini akiwa amezichezea Simba sc na Yanga sc kwa mafanikio makubwa.