Jumamosi kikosi cha Yanga kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Mchezo huo utapigwa saa moja jioni
Bila shaka itakuwa siku nyingine kwa kiungo mshambuliaji Bernard Morrisons kuwaongoza mabingwa hao wa kihistoria kusaka ushindi muhimu
Tangu asajiliwe na Yanga mwezi uliopita, Morrison amekuwa na kiwango bora akifunga mabao mawili na kutoa pasi tatu za mabao
Ni mchezo ambao Yanga itahitaji matokeo ya ushindi hasa baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo uliopita
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amethibitisha kuwa mchezo huo utapigwa uwanja wa Taifa ambapo ametaja viingilio kuwa VIP A ni Tsh15,000/-. VIP B na C ni Tsh10,000/- na Mzunguuko ni Tsh5,000/-
Hii itakuwa mara ya pili kwa Morrison kuikabili Tanzania Prisons msimu huu, alikuwemo kwenye kikosi kilichoikabili timu hiyo mchezo wa kombe la FA (ASFC)
Ni katika mchezo huo ambalo alifanya tukio la kutembea juu ya mpira ambalo video yake ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii