Mastaa wa kikosi cha Yanga sc wanatarajiwa kurudi kambini hii leo baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa aliyekua Rais ya Jmt John Pombe Magufuri.
Mastaa hao walikua wanajifua kambini Avic Town kigamboni lakini waliruhusiwa siku ya Jumatatu na Jumanne kupumzika huku wakipata wasaa wa kumuaga Rais Magufuri aliyefariki machi 17.
Kurejea kwa mastaa hao kunamaanisha kuwa klabu hiyo itakua katika maandalizi kabambe ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kmc huku pia wakitarajiwa kuwavaa Prisons katika mchezo wa kombe la Fa mkoani Sumbawanga.