Friday, May 9, 2025
Home Soka Ya Mkude,Chama Yamalizwa Kisomi

Ya Mkude,Chama Yamalizwa Kisomi

by Sports Leo
0 comments

Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Senzo Masingiza amelimaliza kisomi suala la wachezaji Jonas Mkude,Clatous Chama na Gadiel Michael ambao walikua wanakabiliwa na madai ya utovu wa nidhamu baada ya kukutwa na makosa tofautitofauti yaliyopelekea kukosa michezo ya ligi kuu iliyochezwa kanda ya ziwa.

Mkude na Chama wanadaiwa kuchelewa kuripoti kambini baada ya kuomba ruhusa huku taarifa zikdai wachezaji hao walikwenda kustarehe hali iliyowafanya kuzidiwa na usingizi hivyo kuchelewa ndege ya timu kwenda kanda ya ziwa.

Akizngumzia suala hilo wakati wa tukio la kupokea zawadi kwa wachezaji hao kutoka kwa bosi wa timu hiyo Mo dewji senzo alifafanua hatua zilizochukuliwa na klabu hiyo.

banner

“Hakuna mchezaji aliyeadhibiwa bali walisimamishwa kutokana na madai ya utovu wa nidhamu na nilikutana na wachezaji hao na kuzungumza nao mambo yakaisha.

“Niseme tu, hili si kwa wachezaji pekee kwamba ndiyo wanapaswa kuwa na nidhamu bali kwa wote ili kuisaidia Simba kwenda inavyotakiwa ili mambo yaende kwenye mstari,” alisema Mazingisa.

You may also like

Leave a Comment

Soledad is the Best Newspaper and Magazine WordPress Theme with tons of options and demos ready to import. This theme is perfect for blogs and excellent for online stores, news, magazine or review sites.

Buy Soledad now!

Edtior's Picks

Latest Articles

u00a92022u00a0Soledad.u00a0All Right Reserved. Designed and Developed byu00a0Penci Design.