Connect with us

Soka

Uhuru Asajiliwa Fc Lupopo

Winga wa zamani wa Simba sc na Royal Eagle ya South Afrika Uhuru Selemani amejiunga na timu ya Fc lupopo inayoshiriki ligi kuu nchini Kongo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Uhuru aliyeichezea timu ya taifa ya Tanzania enzi za kocha Marcio Maximo aliondoka Simba sc na kujiunga na timu mbalimbali na kisha kutua Royal Eagle ya nchini Afrika kusini kabla ya kuachana na timu hiyo.

Winga huyo anaingia kwenye historia ya kuwa wachezaji wachache kutoka Tanzania kucheza katika ligi kuu nchini Kongo akiungana na Mbwana Samatta,Thomas Ulimwengu,Mussa Hassan Mgosi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka