Benchi la ufundi la AS Vita chini ya Kocha Florent Ibenge limesema kuwa liko tayari kupokea matokeo yoyote kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya Simba sc itakayofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam
Kocha wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa hawako tayari kujiweka kwenye presha kubwa katika mchezo huo na aina yoyote ya matokeo yatakayopatikana watayapokea.
“Siku zote tumekuwa tukifurahia kucheza na ni furaha kubwa zaidi kucheza na timu kama Simba ambayo ni miongoni mwa timu bora na nzuri Afrika.
“Tulicheza mechi ya kwanza kule DR Congo na tukashindwa kufanya kama tulivyotarajia tukapoteza mchezo hivyo tumekuja hapa tukiamini tukicheza kama tulivyopanga tutapata matokeo tunayoyahitaji.
.